Entertainment

NAIBOI AACHIA RASMI OTERO EP

NAIBOI AACHIA RASMI OTERO EP

Mkali wa muziki nchini Naiboi ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Otero EP.

Otero EP ina jumla ya ngoma tisa za moto na bonus track moja ambazo  zimetayarishwa na maprodyuza kama  Baseman 254, Hamadoo on the Beat pamoja Naiboi mwenyewe.

Lakini pia hitmaker huyo wa “usipime mwanaume” amewashirikisha wakali kama nyashinski, Arrow Boy, Femi One, Truth 254, AY  kutoka Tanzania, na Darrio kutoka Jamaica.

Kupitia ukurasa wake wa instagram naiboi amesema ameachia ep yake hiyo kama zawadi kwa mashabiki zake ambao wamekosa muziki kwa takriban miaka miwili.

Otero EP ni kazi ya kwanza kwa mtu mzima Naiboi tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *