
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Dudu Baya, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli kali inayowalenga wanawake wanaotembelea waganga wa kienyeji kwa masuala ya mahusiano.
Kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Dudu Baya alionya vikali wanaume dhidi ya kuwa katika mahusiano na wanawake wanaotafuta huduma za kishirikina ili kudhibiti au kushikilia wapenzi wao.
“Ogopa sana mwanamke anayeenda kwa waganga (mshirikina), mwanaume ukipata mwanamke wa aina hii ni ngumu kufanikiwa. Utajikuta badala ya kwenda mjini unarudi kijijini,” alisema msanii huyo kwa msisitizo.
Kauli hiyo imezua maoni tofauti kutoka kwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii, baadhi wakimuunga mkono huku wengine wakimtaka kutoa ushahidi au kufafanua zaidi kuhusu madai hayo.
Dudu Baya, ambaye amekuwa akijulikana kwa kauli kali na zenye utata, amewahi pia kujihusisha na kampeni dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na pia kuwaasa wasanii wenzake kuzingatia maisha ya kiroho na kimaadili.
Kwa sasa, bado haijafahamika ikiwa kauli hiyo ilikuwa ya jumla au imelenga mtu fulani, lakini imezidi kuibua hisia mseto miongoni mwa wafuasi wake na jamii