Sports news

Liverpool Mbioni Kumuuza Konaté

Liverpool Mbioni Kumuuza Konaté

Klabu ya Liverpool inatazamia kumuuza beki wake wa kati, Ibrahima Konaté, katika dirisha la usajili la msimu wa joto endapo mchezaji huyo ataendelea kukataa ofa ya mkataba mpya wa kusalia Anfield.

Raia huyo wa Ufaransa ameonyesha nia ya kujiunga na klabu kubwa ya Real Madrid ya Hispania katika dirisha hili la usajili, jambo ambalo limekuwa changamoto kwa Liverpool.

Mkataba wa Konaté na Liverpool unamalizika Juni 30, 2026, na klabu hiyo inahofia kumpoteza mchezaji huyo muhimu bure iwapo hataongezea mkataba wake. Kwa hivyo, uamuzi wa kumuuza msimu huu unachukuliwa kama njia ya kuhakikisha klabu inapata fidia kabla ya mkataba wake kuisha.

Liverpool wanatarajia kupata faida kubwa kutokana na uhamisho huo, huku wakijaribu pia kuweka mipango mbadala ya kuongeza nguvu kwenye nafasi ya beki wa kati msimu ujao.