Entertainment

Harmonize Atoa Shukrani kwa Mashabiki, Aahidi Makubwa Kutoka Konde Gang

Harmonize Atoa Shukrani kwa Mashabiki, Aahidi Makubwa Kutoka Konde Gang

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Harmonize, ameonyesha shukrani zake kwa mashabiki wake duniani kote kufuatia akaunti yake ya Instagram kufikisha wafuasi milioni 3.

Kupitia ujumbe maalum aliouweka mtandaoni, Harmonize amewashukuru mashabiki kwa sapoti ya dhati waliyoitoa tangu alipoanza safari yake ya muziki.

Mbali na hilo, Harmonize alitumia nafasi hiyo pia kutangaza kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu, lebo ya Konde Gang itawatambulisha wasanii wapya wawili, hatua ambayo inalenga kupanua familia ya Konde Gang na kukuza vipaji vipya katika tasnia ya muziki.

Aidha, Harmonize aliwaahidi mashabiki wake kuwa kuna ngoma kali zinazokuja hivi karibuni kabla ya mwezi Agosti, akitaja kuwa ataachia kazi mpya zinazofuatia mafanikio ya nyimbo zake zilizopita.

Mashabiki wake mitandaoni wameonyesha furaha kubwa kwa hatua hiyo, wakimsifia kwa juhudi zake za kukuza muziki wa Bongo Fleva na kulea vipaji kupitia Konde Gang.