LifeStyle

Pritty Vishy Afichua Gharama Halisi za Upasuaji Wake wa Urembo

Pritty Vishy Afichua Gharama Halisi za Upasuaji Wake wa Urembo

Mrembo maarufu wa mitandao ya kijamii nchini Kenya, Pritty Vishy, ameweka wazi gharama kamili alizotumia kubadilisha mwonekano wa mwili wake kupitia upasuaji wa urembo.

Akizungumza kuhusu safari hiyo, Vishy alisema alitumia kati ya KSh 1.2 milioni na KSh 1.5 milioni, kinyume na uvumi ulioenea mitandaoni uliodai alitumia KSh 500,000 pekee.

Upasuaji huo ulihusisha kuboresha makalio kwa mafuta (Brazilian Butt Lift – BBL), kuondoa mafuta ya ziada mwilini (Liposuction), na kuondoa ngozi pamoja na mafuta tumboni (Tummy Tuck).

Alifafanua kuwa sehemu kubwa ya bajeti hiyo ilihusisha Tummy Tuck iliyogharimu kati ya KSh 350,000 na 400,000, Lipo 360 iliyogharimu kati ya KSh 300,000 na 350,000, pamoja na BBL iliyomgharimu KSh 500,000. Gharama hizo pia zilijumuisha huduma za baada ya upasuaji kama vile massages, vifaa muhimu na ukaguzi wa kitabibu.

Vishy aliongeza kuwa alitumia kati ya KSh 400,000 na 500,000 kwa dawa ya Ozempic, inayotumika kudhibiti uzito, jambo lililoongeza zaidi gharama za safari yake ya kubadilisha muonekano.

Kauli yake imeibua mjadala mitandaoni, huku wafuasi wake wakitofautiana kuhusu maamuzi yake na kiwango kikubwa cha fedha alichowekeza katika mwonekano wake wa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *