Entertainment

Khaligraph Jones Athibitisha Kufungwa kwa Mradi wa Khali Cartel

Khaligraph Jones Athibitisha Kufungwa kwa Mradi wa Khali Cartel

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ametangaza kwamba msururu wake wa rap cypher unaotambulika kama Khali Cartel ulimalizika rasmi mwaka jana.

Kupitia Instagram Stories, Khaligraph alijibu shabiki aliyemuuliza kuhusu hatma ya mradi huo, akieleza kuwa Khali Cartel ilitimiza lengo lake kuu la kukuza na kutambulisha wasanii chipukizi kwenye tasnia ya muziki.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018, Khali Cartel imekuwa jukwaa muhimu kwa wasanii wachanga kuonesha umahiri wao wa kurap, huku ikichangia kwa kiasi kikubwa kugundua na kukuza vipaji vipya katika tasnia ya muziki wa hip hop nchini Kenya.

Hata hivyo, Khaligraph hakubainisha iwapo ataanzisha mradi mpya wa aina hiyo, bali alichukua fursa hiyo kuwashukuru mashabiki na wasanii wote waliokuwa sehemu ya safari ya Khali Cartel hadi mwisho wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *