Sports news

Newcastle Yamsajili Malick Thiaw Kutoka AC Milan

Newcastle Yamsajili Malick Thiaw Kutoka AC Milan

Klabu ya Newcastle United imethibitisha kumsajili rasmi beki wa kati wa AC Milan, Malick Thiaw, kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa pauni milioni 30.2, pamoja na marupurupu yanayoweza kufikia pauni milioni 4.3.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, mzaliwa wa Düsseldorf nchini Ujerumani, amejiunga na Newcastle baada ya kipindi cha mafanikio akiwa na miamba wa Italia, AC Milan. Thiaw alijiunga na Milan mwaka 2022 akitokea Schalke 04 ya Bundesliga na ameichezea timu hiyo mechi 85 katika mashindano mbalimbali.

Katika msimu uliopita, Thiaw alikuwa sehemu ya kikosi cha Milan kilichoshinda taji la Supercoppa Italiana kwa kuwacharaza mahasimu wao wa jadi, Inter Milan, katika fainali. Ushindi huo uliifanya Milan kutwaa taji lao la nane la Super Italia.

Thiaw anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Newcastle kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England (EPL), huku kocha wa timu hiyo Eddie Howe akiweka wazi kuwa ni mchezaji aliyekuwa akimfuatilia kwa muda mrefu kutokana na uwezo wake wa kimataifa na uzoefu katika mashindano makubwa ya Ulaya.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *