
Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Guardian Angel, amefichua kiwango kikubwa cha fedha anachotumia kila mwezi kugharamia mahitaji yake ya msingi. Akipiga stori na podcast ya Mwakideu live, Guardian Angel amesema kuwa matumizi yake ya kila mwezi ni zaidi ya Shillingi milioni 1.5.
Kwa mujibu wa msanii huyo, kiasi hicho kinahusisha gharama za maisha, miradi ya muziki, pamoja na majukumu mengine ya kifamilia na kijamii anayobeba. Amebainisha kuwa licha ya muziki wa injili kutoonekana kama sekta yenye mapato makubwa, yeye ameweza kujipanga kimaisha kuhakikisha anadumisha kiwango chake cha maisha.
Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakisifia uaminifu na uthubutu wake wa kuweka wazi hali yake ya kifedha, huku wengine wakishangazwa na ukubwa wa gharama hizo.