LifeStyle

Miss Morgan Afunguka Kuhusu Mapambano na Pombe

Miss Morgan Afunguka Kuhusu Mapambano na Pombe

Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi maarufu cha Tahidi High, Miss Morgan, amefunguka kuhusu safari yake ngumu ya kupambana na msongo wa mawazo pamoja na uraibu wa pombe.

Akizungumza na podcast ya AM Live, Miss Morgan amesema maisha yake yalibadilika sana baada ya kuondoka kwenye kipindi hicho maarufu, huku umaarufu ukipungua na changamoto binafsi zikiongezeka. Amefichua kuwa shinikizo la kudumisha taswira yake mbele ya umma, matatizo ya kifedha na kukatishwa tamaa kimaisha vilimsukuma kuanza kutumia pombe kupita kiasi kama njia ya kukabiliana na hali.

Hata hivyo, ulevi huo uliendelea kukua na kuathiri zaidi afya yake ya akili na mahusiano yake. Amekiri kuwa alifika hatua ya kukata tamaa kabisa na kufikiria kujiua.

Kwa sasa, Miss Morgan anasema anaendelea na safari ya kupona na amejitolea kuhamasisha jamii kuhusu afya ya akili. Anawahimiza wale wanaopitia changamoto kama zake kuzungumza na kutafuta msaada bila kuogopa unyanyapaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *