Sports news

Man United Yagonga Mwamba kwa Dili la Carlos Baleba

Man United Yagonga Mwamba kwa Dili la Carlos Baleba

Klabu ya Manchester United imepata pigo katika juhudi zake za kumsajili kiungo mkabaji wa Brighton, Carlos Baleba, baada ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England kusisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi kwa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Manchester United ilifanya mawasiliano rasmi na Brighton ili kuanza mazungumzo ya kumnasa nyota huyo raia wa Cameroon, lakini Brighton iligoma hata kutaja dau lolote, ikieleza kuwa haina mpango wa kumuachia kabla ya kiangazi cha mwaka 2026.

Licha ya msimamo huo, Carlos Baleba anaripotiwa kuwa na nia ya kujiunga na kikosi cha Manchester United. Hata hivyo, ameweka wazi kuwa hatalazimisha uhamisho huo kwani bado anafurahia maisha yake ya soka ndani ya Brighton.

Kwa sasa, Manchester United italazimika kutazama chaguo jingine la kuongeza nguvu katika safu ya kiungo, huku Brighton wakisisitiza kwamba Baleba ni sehemu ya mipango yao ya muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *