
Desire luzinda ni moja ya wasanii wa kike ambao waliacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda lakini alipata umaarufu zaidi mwaka wa 2018 wakati picha zake za utupu zilivuja mtandaoni.
Lakini maisha yake yalikuja ya kabadilika baada ya kukumbatia ukristo na akahamua kuacha kabisa muziki wa kidunia na kuhamia kwenye muziki wa injili ambapo amekuwa akitumia umaarufu wake kueneza huduma ya Injili maeneo mbali mbali duniani.
Goods ni kwamba Desire Luzinda anatarajiwa kupokezwa tuzo ya heshima na taasisi ya kutoa mafunzo ya biblia ya World Trumpet huko nchini Marekani.
Hitmaker huyo wa “Damn” atapewa tuzo hiyo kwa sababu ya kuwa moja kati ya watu ambao wamechangia pakubwa kubadili maisha ya watu kupitia huduma ya injili.
Desire Luzinda atatunukiwa tuzo hiyo Disemba 12 mwaka wa 2021 huko Texas nchini Marekani