Gossip

Huddah Atoa Vigezo vya Kukutana Naye, Asema Urafiki Ni Shillingi Milioni 1

Huddah Atoa Vigezo vya Kukutana Naye, Asema Urafiki Ni Shillingi Milioni 1

Sosholaiti wa Kenya, Huddah Monroe, ametangaza masharti mapya kwa mashabiki wanaotamani kukutana naye ana kwa ana.

Kwa mujibu wa mpango huo, atatoza Sh50,000 kwa chakula cha mchana cha saa mbili, ambapo saa moja ya ziada imetengwa kwa ajili ya picha na mazungumzo ya kawaida. Hata hivyo, gharama ya chakula haitajumuishwa na mahali pa kukutana patachaguliwa na mhusika mwenyewe.

Huddah ameliita zoezi hili “The Bachelorette,” akieleza kuwa ni nafasi ya kipekee kwa mashabiki kupata muda wake. Ameweka msimamo kuwa hawezi kutoa muda wake bure kwani anauchukulia kama wa thamani, na kwamba kuwa naye kunahitaji gharama.

Mbali na chakula cha mchana, Huddah pia amedokeza uwezekano wa kushirikiana na mashabiki wake kwenye shughuli nyingine za burudani kama michezo, iwapo watakuwa tayari. Amesema nafasi za kuhudhuria zitafunguliwa rasmi kuanzia Jumanne wiki ijayo.

Katika kujibu shabiki mmoja aliyeuliza kuhusu urafiki, Huddah amesisitiza kuwa hata kuwa rafiki naye ni gharama kubwa, akitaja kiwango cha Sh1 milioni kama ada ya urafiki, akisema muda wake binafsi ni wa thamani na haupatikani kirahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *