Entertainment

Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka kwa uchungu kuhusu changamoto alizopitia kabla ya kutamba kwenye muziki, akisimulia namna alivyoachwa na mpenzi wake kwa madai ya kutokuwa na uwezo wa kumuhudumia kifedha.

Akipiga stori na podcast ya Telliswift, Diamond amekiri kuwa maumivu ya kuachwa ndiyo yaliyompa msukumo wa kuandika wimbo “Kamwambie”, uliompa umaarufu mkubwa na kufungua rasmi milango ya mafanikio katika muziki wake. Baada ya kuachia wimbo huo, alijipatia mashabiki lukuki na kufanikisha kushinda tuzo mbalimbali zilizomtambulisha rasmi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Staa huyo amekiri kuwa safari yake haikuwa rahisi, kwani familia yake ilitoka kwenye hali ya umasikini mkubwa na ili kuendeleza ndoto zake, alilazimika kufanya kazi za mikono ili kujikimu kimaisha. Amefichua kwamba aliwahi kuuza nguo za mitumba, kufanya kazi katika kituo cha mafuta, na hata kujihusisha na upigaji picha, kazi ambayo wakati huo ilidharaulika sana.

Hata hivyo, Diamond anasema hajawahi kusahau maumivu yaliyompa motisha ya kuandika wimbo wa “Kamwambie.” uliompa jina. Leo hii, Diamond Platnumz anahesabika kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, lakini safari yake ya kufika hapo imetokana na maumivu, uvumilivu na bidii ya miaka mingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *