Diamond Atoa Mtaji kwa Wafanyibiashara Wadogo kama Zawadi ya Siku ya Valentine’s

Diamond Atoa Mtaji kwa Wafanyibiashara Wadogo kama Zawadi ya Siku ya Valentine’s

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameigeuza Siku ya Wapendanao Duniani kuwa siku ya matumaini kwa wafanyabiashara wadogo nchini kwao Tanzania baada ya kuamua kurudisha mkono kwa jamii. Kupitia video aliyochapisha mitandaoni, Diamond anaonekana akisimamisha gari lake kando ya barabara na kushuka kukutana na kundi la akina mama waliokuwa wakifanya biashara zao ndogo ndogo. Baada ya mazungumzo mafupi, msanii huyo alianza kutoa vibunda vya pesa kwa kila mama kama mtaji wa kuwawezesha kukuza biashara zao. Akina mama hao walionekana kushangazwa na kuguswa mno na kitendo hicho cha upendo, huku wakimshukuru kwa furaha. Wengi wao wameeleza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka na utasaidia kuboresha maisha yao pamoja na familia zinazowategemea.

Read More
 Diamond Amtabiria Binti Yake kuwa Miss World

Diamond Amtabiria Binti Yake kuwa Miss World

Msanii nyota wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz, ametoa kauli inayotafsiriwa na wengi kama utabiri mzuri kwa mustakabali wa binti yake, Tiffah Dangote. Kupitia ukurasa wa Instagram wa Tiffah, Diamond amejibu posti ya binti yake aliyokuwa akielezea nafasi yake katika familia yao kwa maneno mafupi lakini yenye uzito mkubwa akimuita “My Miss World” Kauli hiyo ya Diamond imechukuliwa na mashabiki kama ishara ya matumaini na utabiri mzuri kwa binti huyo, wengi wakiamini kuwa Tiffah ana kila sifa ya kuwa nyota mkubwa siku za usoni, ikiwemo kufikia mafanikio makubwa kama kushiriki mashindano ya kimataifa kama Miss World. Mashabiki wamehusisha kauli hiyo na malezi pamoja na mazingira ya kifamilia anayokulia Tiffah, wakiamini kuwa upendo na sapoti anayopata kutoka kwa baba yake vinaweza kumjenga kuwa kiongozi au nyota mkubwa wa baadaye, ikiwemo kufikia ndoto kubwa kama kushiriki mashindano ya kimataifa ya urembo kama Miss Dunia.

Read More
 Diamond Adaiwa Kumtelekeza Mkubwa Fella akiwa Mgonjwa

Diamond Adaiwa Kumtelekeza Mkubwa Fella akiwa Mgonjwa

Mke wa Mkubwa Fella, ameibuka na madai mazito dhidi ya Diamond Platnumz akisema kuwa kwa sasa staa huyo wa muziki amewazimia kabisa simu liicha ya kujaribu kuwasiliana naye mara kadhaa bila mafanikio. Akizungumza kwa masikitiko, mke huyo amesema kuwa Diamond hajibu simu wala meseji wanazomtumia, hata katika kipindi hiki ambacho mume wake, Mkubwa Fella, anaumwa. Amesema hali hiyo imewawavunja moyo, hasa ikizingatiwa kuwa ni Fella mwenyewe anayempigia Diamond lakini hajibiwi kabisa. Ameeleza kuwa mara ya mwisho Diamond Platnumz kuonyesha msaada kwa familia hiyo ilikuwa mwaka jana walipompeleka Fella nchini India kwa ajili ya matibabu. Kwa mujibu wa mke huyo, kinachoumiza zaidi ni historia ndefu ya uhusiano kati ya Diamond na Mkubwa Fella, ambapo meneja huyo alisimama naye katika nyakati ngumu za mwanzo wa safari yake ya muziki. Mkubwa Fella anatajwa kuwa miongoni mwa watu waliomshika mkono Diamond, hasa kipindi ambacho baadhi ya vyombo vya habari vilikataa kupiga nyimbo zake.

Read More
 Diamond Platnumz Awajibu Wakosoaji kwa Begi Lililojaa Dola za Kimarekani

Diamond Platnumz Awajibu Wakosoaji kwa Begi Lililojaa Dola za Kimarekani

Msanii nyota Barani Afrika, Diamond Platnumz, amezua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya hatua yake ya kuonekana kuwajibu wale waliodai kususia muziki wake kutokana na masuala ya kijamii na kisiasa yaliyoibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki. Kupitia Instagram Story yake, Diamond ameshare video fupi akionyesha begi lililojaa Dola za Kimarekani akiwa ndani ya ndege huku akiambatanisha na wimbo wake wa Sasampa aliyowashirikisha wasanii Focalistic, Uncool MC, Silas Africa, na Xduppy, wote wanatoka Afrika Kusini. Katika video hiyo, Diamond anaonekana akihesabu maelfu ya dola na msaidizi wake, hatua ambayo imechukuliwa na wengi kama ujumbe wa moja kwa moja kwa wanaodai kususia kazi zake kwa madai ya kujihusisha na siasa zilizotumbukiza Tanzania kwenye machafuko baada ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Licha ya mjadala huo, Diamond Platnumz anaendelea kubaki miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, si tu kupitia muziki wake bali pia kupitia miradi yake ya kibiashara. Tu

Read More
 Diamond Aingilia Ndoa ya Mwijaku

Diamond Aingilia Ndoa ya Mwijaku

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameamua kuingilia kati sakata la ndoa ya mtangazaji na mwanahabari Mwijaku, ambayo kwa sasa inadaiwa kuyumba kufuatia madai ya usaliti. Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Diamond ameonekana akiwa pamoja na Mwijaku ambapo alitumia fursa hiyo kumuomba msamaha mke wa Mwijaku na kumshawishi arejee nyumbani ili kuokoa ndoa yao. Diamond amemhimiza Mwijaku kutatua tofauti zilizopo kati yake na mkewe badala ya kufikiria kuachana, akisisitiza kuwa ndoa inahitaji uvumilivu na msamaha. Ameeleza kuwa mke wa Mwijaku ni mtu wa thamani ambaye wameishi naye kwa amani kwa muda mrefu, hivyo haifai kuvunja ndoa kwa sababu ya changamoto. Akizungumza kwa hisia, Diamond amesisitiza kuwa wamepitia kipindi kigumu sana kama familia na marafiki, na akaomba kwa unyenyekevu mke wa Mwijaku amsamehe mumewe kwa ajili ya mustakabali wa familia yao. Hatua hiyo ya Diamond imekuja baada ya mke wa Mwijaku kuripotiwa kumkimbia mumewe, hali iliyozua gumzo kubwa mitandaoni.

Read More
 Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameibua gumzo baada ya kuwatolea uvivu watu wanaoendelea kulalamikia serikali kuhusu hali ya maisha. Kupitia ujumbe wake, Diamond amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuongeza bidii kwenye kazi zao badala ya kuishia kuilaumu serikali kila mara. Hitmaker huyo wa Mtasubiri ameongeza kuwa changamoto za maisha ni za kawaida, na anayejituma hupata matunda yake bila kujali nani yupo madarakani. Diamond, ambaye mara nyingi hujitokeza kuzungumzia masuala ya kijamii, amesema ataendelea kuwatia moyo vijana kufanya kazi kwa bidii na kutumia vipaji vyao ipasavyo ili kuondokana na utegemezi. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono kwa kusema ujumbe huo ni wa kuhamasisha, huku wengine wakihisi amewabeza wananchi wanaopitia ugumu wa maisha.

Read More
 Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Diamond Platnumz Asema Maumivu ya Mapenzi Yalimjengea Ustaa

Mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefunguka kwa uchungu kuhusu changamoto alizopitia kabla ya kutamba kwenye muziki, akisimulia namna alivyoachwa na mpenzi wake kwa madai ya kutokuwa na uwezo wa kumuhudumia kifedha. Akipiga stori na podcast ya Telliswift, Diamond amekiri kuwa maumivu ya kuachwa ndiyo yaliyompa msukumo wa kuandika wimbo “Kamwambie”, uliompa umaarufu mkubwa na kufungua rasmi milango ya mafanikio katika muziki wake. Baada ya kuachia wimbo huo, alijipatia mashabiki lukuki na kufanikisha kushinda tuzo mbalimbali zilizomtambulisha rasmi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva. Staa huyo amekiri kuwa safari yake haikuwa rahisi, kwani familia yake ilitoka kwenye hali ya umasikini mkubwa na ili kuendeleza ndoto zake, alilazimika kufanya kazi za mikono ili kujikimu kimaisha. Amefichua kwamba aliwahi kuuza nguo za mitumba, kufanya kazi katika kituo cha mafuta, na hata kujihusisha na upigaji picha, kazi ambayo wakati huo ilidharaulika sana. Hata hivyo, Diamond anasema hajawahi kusahau maumivu yaliyompa motisha ya kuandika wimbo wa “Kamwambie.” uliompa jina. Leo hii, Diamond Platnumz anahesabika kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, lakini safari yake ya kufika hapo imetokana na maumivu, uvumilivu na bidii ya miaka mingi.

Read More
 Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Diamond Platnumz Aingilia Mzozo Kati ya Babalevo na Mbosso

Mzozo ulioshika kasi mitandaoni kati ya Babalevo na Mbosso kuhusu wimbo ‘Pawa’ umechukua mwelekeo mpya baada ya Diamond Platnumz kuingilia kati na kutoa msimamo wake. Babalevo na Mbosso walikuwa wakijibizana mitandaoni huku jina la Diamond likihusishwa kwenye malumbano hayo. Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ametoa kauli ya kutaka pande zote mbili kumheshimu, akisisitiza kuwa amekuwa akiwaheshimu na hana sababu ya kuhusishwa na migogoro yao. Diamond alimueleza Babalevo kuwa licha ya kumheshimu kama kijana mwenzake, maneno na mienendo yake yameanza kumpa hisia za kutilia shaka, hali inayoweza kupelekea kutojihusisha naye. Aidha, alimkumbusha Mbosso kuwa ana haki ya kukasirika au kujibu pale anapojisikia amekosewa, lakini akamtaka asiingize jina lake katika malumbano hayo, jambo ambalo amesema wameshazungumzia mara kadhaa huko nyuma. Hitimisho la ujumbe wake lilikuwa wito wa kuheshimiana, akieleza kwamba ikiwa wawili hao wana ajenda tofauti wanazopanga kupitia kivuli chake, basi waendelee, ila yeye hatashiriki.

Read More
 Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Diamond Platnumz Asema Hana Msemaji Rasmi

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Juma, maarufu kama Diamond Platnumz, ametoa tamko rasmi akieleza kuwa hajawahi na hajateua mtu yeyote kuwa msemaji wa maisha yake binafsi au kazi zake za muziki. Kupitia taarifa hiyo, Diamond amesisitiza kuwa taarifa yoyote inayotolewa na mtu mwingine kwa niaba yake haina uhalali wowote na haitakiwi kuchukuliwa kama ya kweli. Ameeleza kuwa iwapo mtu yeyote ataamua kuamini taarifa hizo zisizo rasmi, basi matokeo ya imani hiyo yatakuwa juu ya mhusika mwenyewe, na yeye hatalaumiwa kwa lolote linalotokana na hilo. Ameweka wazi kuwa endapo kutakuwa na jambo lolote muhimu la kuzungumza, atazungumza mwenyewe kupitia njia rasmi bila kumtuma mtu yeyote kumwakilisha. Mashabiki na vyombo vya habari wanahimizwa kufuatilia vyanzo rasmi vya mwanamuziki huyo kwa taarifa sahihi na kuepuka upotoshaji. Tamko hili limekuja kufuatia hali ya sintofahamu iliyojitokeza kwa muda sasa, ambapo Baba Levo amekuwa akizungumza mara kwa mara kuhusu maisha ya ndani ya Diamond na kazi zake, hali iliyowafanya baadhi ya watu kumchukulia kama msemaji wake wa karibu.

Read More
 Diamond Apuuzilia Madai ya Wasanii wa Bongo Kukosa Dili za Kimataifa

Diamond Apuuzilia Madai ya Wasanii wa Bongo Kukosa Dili za Kimataifa

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameonesha kutoridhishwa na hatua ya jina na picha yake kutumiwa na ukurasa maarufu wa mitandaoni nchini kwao, katika mjadala kuhusu kwa nini wasanii wa Tanzania hushindwa kusainiwa na lebo kubwa za kimataifa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amejibu vikali mada hiyo, akieleza kuwa amekuwa na mafanikio makubwa katika anga za kimataifa. Amesema amewahi kupokea ofa kutoka kwa lebo kubwa duniani kama Universal Music Group na Roc Nation, na hatimaye alisaini mkataba rasmi na Warner Music, unaokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 13.5 za Kitanzania. Msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa lebo ya WCB Wasafi, amesema mafanikio yake hayakuja kwa bahati bali ni matokeo ya bidii, maadili ya kazi na kujituma kwake. Ametaja kuwa amewahi kushirikiana na mastaa wa kimataifa kama Alicia Keys, Rick Ross, Ne-Yo, Omarion na wengine wengi, ishara kuwa anaheshimiwa na kutambuliwa hata nje ya mipaka ya Afrika. Kauli hiyo imeibua mjadala mpana mitandaoni, huku mashabiki wake wakimtetea vikali, wakisisitiza kuwa Diamond ni miongoni mwa wasanii wachache barani Afrika walioweza kuvuka mipaka ya bara na kupata nafasi katika jukwaa la kimataifa.

Read More
 Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Victoria Kimani Akanusha Kumlenga Diamond Katika Kauli Yake ya Rolls Royce

Msanii wa muziki wa R&B kutoka Kenya, Victoria Kimani, hatimaye amejibu ukosoaji ulioibuka baada ya mahojiano yake kwenye Mic Cheque Podcast, ambako alitoa kauli iliyotafsiriwa na wengi kuwa ni dongo kwa msanii nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz. Katika mahojiano hayo, Kimani alidai kuwa kuna Rolls Royce ya rangi ya buluu inayodaiwa kuwa ya bandia, kauli ambayo iliwafanya mashabiki wengi kuamini kuwa alikuwa akimlenga Diamond, ambaye hivi majuzi alijivunia kumiliki gari hilo la kifahari. Hata hivyo, akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Milard Ayo, Victoria Kimani alikanusha madai hayo kwa kusisitiza kuwa hakuwa amemtaja mtu yeyote kwa jina. “Sikutaja jina la mtu yeyote… acheni. Nilisema nilichosema, haikuwa maana ya ndani,” alisema Kimani kwa msisitizo. Kauli hiyo ya Kimani imeibua mjadala mkali mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimtetea kwa kusema ana uhuru wa kutoa maoni yake, na wengine wakimtaka awe makini na matamshi yake, hasa inapohusiana na wasanii wengine wakubwa wa Afrika Mashariki. Diamond Platnumz hajatoa tamko rasmi kuhusiana na madai hayo, huku baadhi ya mashabiki wake wakimtetea vikali kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki sasa wanasubiri kuona iwapo kutakuwa na mwendelezo wa mvutano huu au kama pande zote zitapuuza na kuendelea na kazi zao za kisanaa.

Read More
 Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Victoria Kimani Amrushia Dongo Diamond Platnumz: Adai Rolls Royce ya Buluu Ni ya Bandia

Mwanamuziki na mtunzi mashuhuri Victoria Kimani amezua gumzo mitandaoni baada ya kudokeza kuhusu gari la kifahari aina ya Rolls Royce linalodaiwa kuwa la bandia, ambalo linapigiwa debe katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Victoria alirusha dongo la chinichini kwa mtu mashuhuri ambaye hakumtaja moja kwa moja, akidai kuwa anajigamba na gari la kifahari lisilo halisi. “Si kila Rolls Royce ya buluu unayoiona mitaani ni halisi. Wengine wanapenda kuishi kwa kiki kuliko uhalisia,” alisema Kimani. Ingawa hakumtaja jina mhusika, mashabiki na wachambuzi wa mitandao walihisi kuwa ujumbe huo umeelekezwa kwa kwa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameonekana mara kwa mara akipiga picha na gari la kifahari la rangi ya buluu katika hafla mbalimbali. Kauli ya Kimani imezua maoni mseto, baadhi wakimpongeza kwa kusema ukweli huku wengine wakimshutumu kwa kuanzisha mzozo usio na msingi. Wafuasi wa Diamond wamemkingia kifua msanii wao, wakisisitiza kuwa gari hilo ni halisi na lilinunuliwa kihalali. Diamond Platnumz bado hajajibu hadharani kuhusu suala hilo, lakini mijadala inaendelea kushika kasi mitandaoni huku mashabiki wakingoja kuona iwapo atatoa majibu au kulipuuza kabisa.

Read More