Entertainment

Mashabiki Wamtaja Rigathi kwenye Kauli ya YY Comedian Kuhusu Kipigo cha Harambee Stars

Mashabiki Wamtaja Rigathi kwenye Kauli ya YY Comedian Kuhusu Kipigo cha Harambee Stars

Mchekeshaji YY Comedian ameonyesha masikitiko yake kufuatia timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, kuondolewa na Madagascar katika robo fainali ya michuano ya CHAN 2024.

YY, kupitia ukurasa wake wa Instagram, amedai huenda kulikuwa na bahati mbaya iliyosafirishwa kutoka nje ya nchi na mtu fulani, akitilia shaka matokeo hayo kwa kuzingatia rekodi nzuri ya Kenya kwenye michezo ya awali.

Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni baada ya mashabiki kuhusisha dondoo za mchekeshaji huyo na kurejea kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutoka Marekani siku moja kabla ya mechi, ambapo alihudhuria pambano hilo pamoja na mashabiki wengine wa Kenya.

Kenya ilipoteza kwa mikwaju ya penalti 4-3, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, matokeo yaliyokatisha matumaini ya mashabiki waliokuwa na imani kubwa kwa Harambee Stars kufika hatua za juu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *