
Sosholaiti maarufu wa Kenya, Vera Sidika, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kumtolea uvivu mchekeshaji Mammito Eunice kufuatia kauli yake kuhusu upasuaji wa kuongeza makalio (BBL).
Mammito alikuwa ametupa dongo akidai wanawake wengi kutoka jamii ya Luhya wanapendelea sana urembo wa upasuaji, jambo ambalo halikumpendeza Vera. Kupitia Instastory yake, Vera alimjibu kwa kejeli, akimshambulia binafsi na kumshauri akubaliane na hali yake.
“The fact hauna pesa ya BBL inashangaza. Please embrace your bones in peace.”, Aliandika Inststory
Majibizano hayo yamezua mjadala mkubwa mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimpongeza Vera kwa kujiamini, huku wengine wakimkosoa kwa kutumia maneno ya kudhalilisha.
Tukio hili lilitokea wakati Vera akijaribu kukanusha madai ya wakosoaji waliokuwa wakipotosha kuhusu uhalali wa gari lake la kifahari aina ya Range Rover, ambalo alilishiriki kwenye ukurasa wake wa Instagram.