
Msanii wa muziki kutoka Pwani, Nyota Ndogo, ametoa mtazamo wake kuhusu ndoa na uhusiano. Kupitia ujumbe aliouchapisha, alisema kuwa kwake binafsi, anaona ni bora mwanamke aolewe na mwanaume ambaye ameachana na mke wake kwa talaka, kuliko mwanaume ambaye amempoteza mke kwa kifo.
Kwa mujibu wake, mwanaume ambaye ameachana na mke wake mara nyingi huwa tayari kuanza ukurasa mpya, tofauti na yule aliyefiwa na mke, ambaye kumbukumbu na mapenzi ya mke aliyefariki hubaki moyoni na mara nyingi huathiri ndoa mpya.
Baadhi ya mashabiki walikubaliana naye wakisema ni vigumu kushindana na kumbukumbu ya mke aliyefariki, huku wengine wakimkosoa wakidai kuwa kifo hakimaanishi mtu amekwama katika maisha ya ndoa, kwani anaweza kumpenda na kumheshimu mke mpya bila matatizo.
Nyota Ndogo mara kwa mara hutoa maoni ya moja kwa moja kuhusu masuala ya ndoa na mahusiano, na amesema huwa anazungumza kile anachoamini bila kuficha hisia zake.