Tech news

Google Yazindua “Calling Card” Kwa Watumiaji wa Android

Google Yazindua “Calling Card” Kwa Watumiaji wa Android

Google imeanza kutekeleza mabadiliko mapya yanayolenga kuboresha uzoefu wa watumiaji wa Android, hususan katika eneo la kupiga na kupokea simu. Kupitia sasisho jipya, watumiaji sasa wanaweza kubadilisha mwonekano wa call screen kwa kutumia kipengele kipya kinachoitwa “Calling Card.”

Kupitia Calling Card, mtumiaji anaweza kuchagua aina ya herufi za jina, rangi mbalimbali, picha ya full screen, na kubadilisha jinsi skrini ya simu inavyoonekana pale mtu anapopiga simu. Hii inamaanisha kuwa sasa kila simu inayoingia inaweza kuwa na mwonekano wa kipekee wa kuvutia na wa kibinafsi zaidi.

Mabadiliko haya mapya yanaifanya Android kufanana zaidi na mfumo wa iOS wa Apple, ambao kwa muda mrefu umejulikana kwa muonekano wake wa kuvutia wa skrini ya simu za kuingia. Kupitia hatua hii, Google inaonyesha nia yake ya kuleta ubunifu unaowapa watumiaji uhuru zaidi wa kubinafsisha vifaa vyao.

Kwa sasa, kipengele hiki kinapatikana kwa baadhi ya watumiaji na kinatarajiwa kusambaa zaidi kwa njia ya update ya Google Phone app katika wiki zijazo.

Watumiaji wa Android wanashauriwa kuhakikisha programu zao ziko katika toleo jipya kabisa ili kupata huduma hii mpya ya kuvutia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *