
Mwigizaji wa Kenya, Jackie Matubia, hatimaye amevunja ukimya wake kufuatia madai mazito yaliyomhusisha na kuvunjika kwa ndoa ya mwanamke mmoja.
Akizungumza baada ya sakata hilo kusambaa mitandaoni, Matubia amekanusha madai hayo, akisema hayana msingi wowote. Ameeleza kuwa taarifa hizo zilibuniwa kwa lengo la kumchafua na kumharibia jina mbele ya mashabiki wake na umma kwa ujumla.
Mrembo huyo amesema kwamba kama kweli angekuwa amenunuliwa gari na nyumba na mume wa mwanamke huyo, asingekuwa katika hali ya kuhangaika kila siku kutafuta kipato cha kuendesha maisha yake.
Hata hivyo, Matubia amewataka Wakenya kutoamini taarifa hizo, akisisitiza kuwa zinaenezwa kwa nia ya kumvunjia heshima.
Wiki hii, mwanamke mmoja kupitia Instagram Stories za bloga Edgar Obare, alimtuhumu Matubia kwa kuwa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake. Mwanamke huyo alidai kuwa wakati Matubia akiigiza kwenye kipindi cha Zora, alihusiana kimapenzi na mume wake, ambaye pia alinaswa akihusishwa na Shirika la Ujasusi (NIS).
Hata hivyo, Matubia amewataka Wakenya kutoamini taarifa hizo, akisisitiza kuwa zinaenezwa kwa nia ya kumvunjia heshima. Tukio hili limeendelea kuzua gumzo mitandaoni huku mashabiki wakisubiri kuona hatua atakazochukua dhidi ya madai hayo.