
Rapa Khaligraph Jones, ametangaza kuwa anatamani kununua tena gari lake la zamani aina ya Subaru Forester ambalo liliwahi kuwa sehemu ya maisha yake kabla ya kupata umaarufu mkubwa.
Khaligraph ameeleza kupitia mitandao ya kijamii kuwa anataka kulipata tena Subaru hilo, akiwataka mashabiki wanaofahamu lilipo kumjulisha.
Hatua hiyo imezua hisia tofauti mitandaoni, wengi wakikumbuka jinsi gari hilo lilivyokuwa sehemu ya safari yake ya muziki kabla ya kupata mafanikio makubwa
Tangazo hili linakuja wiki chache baada ya rapa wa Marekani, Rick Ross, kusema bado anamiliki BMW iliyotumika kwenye video ya wimbo wake maarufu Hustlin’ zaidi ya miaka 15 iliyopita.
Wadadisi wa muziki wanasema hatua ya Khaligraph huenda ni jaribio la kuonyesha kuthamini safari yake ya muziki na mafanikio aliyopata tangu siku za mwanzo.