Entertainment

Cardi B Kortini! Akanusha Kumshambulia Mlinzi Akiwa Mjamzito

Cardi B Kortini! Akanusha Kumshambulia Mlinzi Akiwa Mjamzito

Rapa wa Marekani, Cardi B, amekanusha vikali madai kwamba alimshambulia mlinzi wa usalama mwaka 2018 wakati akiwa mjamzito.

Akiwasili mahakamani mjini Alhambra, California siku ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, jana, Cardi amesema hakuwahi kumgusa mlalamikaji Emani Ellis na kudai madai hayo hayana ukweli wowote. Msanii huyo amesisitiza kwamba Ellis ndiye aliyekuwa akimfuata na hata kujaribu kumrekodi bila ridhaa, jambo ambalo lilimfanya ahisi kuvamiwa faragha yake.

Ellis, ambaye aliwasilisha ushahidi wake Jumatatu, anadai kuwa Cardi alimtukana, kumtupia mate, kumwekea kidole usoni na kuamuru walinzi wake kumshikilia katika ofisi ya daktari wa kina mama mwezi Februari mwaka 2018. Ellis amemshtaki Cardi kwa shambulio na kupiga, kusababisha msongo wa mawazo, uzembe na kizuizi cha kiholela.

Kupitia kesi hiyo ya madai, Ellis anataka fidia ya gharama za matibabu, malipo ya mapato aliyopoteza na atakayopoteza siku zijazo, pamoja na adhabu ya kifedha na faini ya kiraia ya $25,000, kwa mujibu wa CourtTV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *