LifeStyle

Terence Creative Atoa Ushauri kwa Wasanii Kuhusu Maisha ya Baada ya Muziki

Terence Creative Atoa Ushauri kwa Wasanii Kuhusu Maisha ya Baada ya Muziki

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Terence Creative, amewashauri wasanii wenzake kujiandaa kwa maisha ya baadaye akionya kwamba taaluma ya sanaa, hususan muziki, haiwezi kudumu milele.

Kupitia ujumbe wake, Terence amesema ni muhimu kwa wasanii kufikiria zaidi ya umaarufu wa sasa na kutengeneza misingi imara ya maisha. Amewashauri kujiwekea akiba, kuwekeza kwenye mali kama ardhi na nyumba, na pia kufungua biashara za pembeni zitakazowawezesha kuwa na kipato cha kudumu hata wakati ambapo muziki au kazi ya sanaa haitawaletea mapato makubwa tena.

Aidha, Terence amewahimiza wasanii kujali afya zao kwa kupata bima ya afya, na pia kupanga mustakabali wa familia zao kwa kuhakikisha watoto wao wana usalama wa kifedha na elimu bora.

Ujumbe wake umewagusa mashabiki na wasanii wengi, huku ukionekana kama wito wa uwajibikaji na kutafakari juu ya maisha ya baadaye. Terence Creative amekuwa mstari wa mbele si tu katika kuleta burudani, bali pia katika kutoa mafunzo ya kijamii kupitia ucheshi na ushauri wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *