LifeStyle

Eve Mungai Afunguka Kuhusu Mapambano ya Afya ya Akili

Eve Mungai Afunguka Kuhusu Mapambano ya Afya ya Akili

Mwanahabari wa kidijitali na mtayarishaji wa maudhui, Eve Mungai, amefunguka kuhusu maisha yake ya ndani kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kigumu alichopitia mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Eve ameeleza kwamba kati ya mwezi Aprili na Juni, alipitia kipindi cha msongo wa mawazo (depression) kikali kilichomfanya kutumia muda mwingi kitandani, kushindwa kula ipasavyo, na kuhisi amelemewa na maisha.

Mrembo huyo, amekiri kuwa maombi, msaada wa familia, marafiki wa karibu na utafutaji wa msaada kitaalamu vilimsaidia hatua kwa hatua kurejea kwenye hali ya kawaida na kupona.

Akizungumzia maisha yake ya kibinafsi, Eve Mungai pia amethibitisha kwamba kwa sasa yupo single, na kufutilia mbali tetesi kuhusu maisha yake ya mahusiano.

Kuhusu hatua yake ya kujiondoa kwenye mahojiano ya mastaa na podcast, Eve amesema baada ya miaka mitano ya kufanya kazi hiyo bila kupumzika, alihisi kuchoka kwa kuwa alikuwa akifukuza ndoto za watu wengine badala ya kuwekeza kwenye ndoto zake binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *