Gossip

Brown Mauzo Aibua Mjadala Kuhusu Single Parents

Brown Mauzo Aibua Mjadala Kuhusu Single Parents

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Brown Mauzo, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kueleza mshangao wake kuhusu ongezeko kubwa la wazazi wanaolea watoto pekee bila wenza.

Kupitia hadithi zake za Instagram, Mauzo alionyesha kushangazwa na namna idadi ya single parents inavyozidi kupanda kila siku. Alisema hali hiyo imeibua swali kubwa kuhusu nani wa kulaumiwa katika changamoto hiyo, ikiwa ni wanaume au wanawake.

Kauli hiyo imezua maoni tofauti mitandaoni, hasa ikizingatiwa kwamba Mauzo mwenyewe ana watoto na wake watatu tofauti (baby mamas). Wapo waliomuunga mkono wakiamini ametaja tatizo halisi la kijamii, huku wengine wakimshutumu wakidai historia yake binafsi inamnyima nafasi ya kutoa ushauri au maoni katika mjadala huo.

Mjadala huu unaendelea kuibua maoni mseto kuhusu familia na malezi ya watoto, na unaonyesha jinsi suala la single parenting linavyoendelea kuchukua nafasi kubwa katika jamii ya sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *