Entertainment

Suge Knight Adai Cheni ya Tupac Aliyonunua Drake Ni Bandia

Suge Knight Adai Cheni ya Tupac Aliyonunua Drake Ni Bandia

Aliyekuwa CEO wa Death Row Records, Suge Knight, ameibua madai makali akiwa jela kuhusu cheni ambayo rapa maarufu Drake alinunua kwa bei ya juu akiamini ilikuwa ya marehemu Tupac Shakur.

Katika mahojiano aliyofanya akiwa gerezani, Suge alifichua kuwa cheni hiyo si halisi, akidai ni bandia (fake) na siyo ile aliyowahi kumpa Tupac kama zawadi enzi za uhai wake.

Suge Knight alisema ana uhakika kwa sababu ndiye aliyemzawadia Tupac cheni ya asili, hivyo anajua kwa undani muonekano na maelezo yake ya kweli. Kwa kauli yake, anakanusha vikali uhalali wa cheni iliyouzwa kwa Drake, jambo linalotilia shaka historia ya thamani inayodaiwa kuambatana nayo.

Kwa mujibu wa taarifa, Drake alinunua cheni hiyo kupitia Alexander Bitar, mtafutaji na muuzaji maarufu wa bidhaa za kihistoria, kwa gharama inayokadiriwa kuanzia $500,000 au zaidi. Cheni hiyo, yenye nembo ya Death Row, imekuwa ikihusishwa moja kwa moja na Tupac kutokana na picha na video zake maarufu akiivaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *