Entertainment

Zuchu Apewa Heshima Kutumbuiza Kwenye Fainali za CHAN 2025 Kenya

Zuchu Apewa Heshima Kutumbuiza Kwenye Fainali za CHAN 2025 Kenya

Msanii maarufu wa Tanzania, Zuchu, ameteuliwa kuwa msanii kinara atakayetumbuiza kwenye sherehe za kufunga mashindano ya CHAN 2025 yatakayofanyika wikiendi hii katika Uwanja wa Moi International Sports Centre, Kasarani jijini Nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alieleza furaha yake akitangaza kuwa atakuwa msanii mkuu wa burudani kwenye fainali hizo, hatua ambayo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake barani Afrika na kwingineko.

Tangazo hilo pia liliibua pongezi kutoka kwa mastaa wa muziki, akiwemo Diamond Platnumz, ambaye alionyesha kufurahishwa na mafanikio ya mpenzi wake na kueleza kuwa hatua hiyo ni kubwa na inamfanya ajivunie zaidi.

Sherehe za kufunga mashindano zinatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kabla ya mchezo wa fainali utakaozikutanisha timu za Morocco na Madagascar Jumamosi, tarehe 30 Agosti 2025, ambapo mshindi atavikwa taji la ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *