Entertainment

Willy Paul Akosoa Waandaaji wa CHAN kwa Kupuuza Wasanii wa Kenya

Willy Paul Akosoa Waandaaji wa CHAN kwa Kupuuza Wasanii wa Kenya

Msanii wa Kenya, Willy Paul, ameibua maswali kuhusu uteuzi wa wasanii waliopangwa kutumbuiza katika fainali ya Mashindano ya CHAN 2024 yatakayofanyika leo Jumamosi katika uwanja wa Kasarani ambapo Morocco itachuana na Madagascar.

Kupitia Instastory,Willy Paul ameonekana kutoridhishwa na uteuzi huo, akidokeza kuwa waandaaji huenda walipuuzia nafasi ya kuhusisha wasanii wengine wa Kenya ambao wangeweza kupeperusha bendera ya taifa ipasavyo kwenye tukio hilo kubwa.

Kauli ya Willy Paul sasa imechochea mjadala mitandaoni kuhusu nafasi ya wasanii wa Kenya katika matukio ya kimataifa, huku baadhi ya mashabiki wakihisi kuwa nchi inapaswa kupewa nafasi kubwa zaidi kupitia muziki wake kwenye majukwaa ya aina hii.

Hayo yote yaliibuka muda mfupi baada ya waandaaji wa mashindano hayo kutangaza kuwa Savara wa Sauti Sol, nyota wa Tanzania Zuchu, na mshindi wa tuzo za kimataifa kutoka Uganda Eddy Kenzo, sio tu watatumbuiza siku ya fainali, bali pia wameandaa na kuimba anthem rasmi ya CHAN 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *