Entertainment

Mariga: Bahati Anatafuta Kiki, Sio Kusaidia Harambee Stars

Mariga: Bahati Anatafuta Kiki, Sio Kusaidia Harambee Stars

Naibu Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Kenya (FKF), McDonald Mariga, ameibua maswali kuhusu ahadi ya msanii Bahati ya kutoa KSh 1 milioni kwa wachezaji wa Harambee Stars.

Kwenye mahojiano na SPM Buzz, Mariga amesema licha ya Bahati kutangaza hadharani mchango huo, hajawahi kuwasilisha fedha hizo kwa wachezaji kama alivyoahidi. Ameeleza pia kutoridhishwa na tabia ya msanii huyo kuanika ahadi kubwa mitandaoni bila utekelezaji, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinaashiria zaidi kutafuta umaarufu badala ya kusaidia timu.

Hali hii inajiri baada ya Bahati kudai kwamba Mariga anahujumu mchakato wa kuzikabidhi pesa hizo kwa wachezaji wa Harambee Stars kwa kutochukua simu zake. Mariga, kwa upande wake, anashikilia kuwa msanii huyo hana nia ya dhati ya kutimiza ahadi hiyo, na kwamba hatua yake ni ya kujitafutia kiki.

Ahadi hiyo ya Bahati ilitolewa wiki kadhaa iliyopita baada ya Harambee Stars kushinda mechi muhimu, ambapo alitangaza kuwa angechangia kiasi hicho kama motisha kwa wachezaji. Hata hivyo, kauli zinazokinzana kati ya pande hizi mbili sasa zimezua sintofahamu na mjadala mkali miongoni mwa mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *