Entertainment

Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Diamond Awataka Watanzania Waache Lawama kwa Serikali

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameibua gumzo baada ya kuwatolea uvivu watu wanaoendelea kulalamikia serikali kuhusu hali ya maisha.

Kupitia ujumbe wake, Diamond amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuongeza bidii kwenye kazi zao badala ya kuishia kuilaumu serikali kila mara.

Hitmaker huyo wa Mtasubiri ameongeza kuwa changamoto za maisha ni za kawaida, na anayejituma hupata matunda yake bila kujali nani yupo madarakani.

Diamond, ambaye mara nyingi hujitokeza kuzungumzia masuala ya kijamii, amesema ataendelea kuwatia moyo vijana kufanya kazi kwa bidii na kutumia vipaji vyao ipasavyo ili kuondokana na utegemezi.

Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakimuunga mkono kwa kusema ujumbe huo ni wa kuhamasisha, huku wengine wakihisi amewabeza wananchi wanaopitia ugumu wa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *