
Mchekeshaji maarufu Eric Omondi ameonyesha moyo wa kusaidia baada ya kujitokeza kumsaidia msanii wa Gengetone, Shalkido, ambaye hivi karibuni alifichua kuwa maisha yamekuwa magumu kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya familia yake.
Mchekeshaji huyo amemkabidhi Shalkido pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya nyumbani ikiwemo unga, sukari na mafuta ya kupikia. Kupitia msaada huo, Eric amesema lengo lake ni kuhakikisha msanii huyo anapata fursa ya kujiinua na kujitegemea tena.
Shalkido, anayejulikana zaidi kupitia kundi la Sailors, amepokea msaada huo kwa furaha na shukrani, akisema utampa nafasi ya kurudia katika mstari sahihi wa kujikimu kimaisha.
Kitendo cha Eric kimepongezwa na mashabiki wengi mitandaoni wakimtaja kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine na jamii kwa ujumla.