
Ngoma mpya ya Diana Marua “Bibi Ya Tajiri” imezua mjadala mkubwa baada ya msanii huyo kutumia sample ya wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, “Saree”.
Ingawa baadhi ya mashabiki waliona hatua hiyo kama heshima kwa nguli huyo wa rap aliyefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita, wengi wameibuka na ukosoaji mkali. Wanasema Diana hana uwezo wa kuchana kama E-Sir na kwamba kutumia ngoma hiyo ni sawa na kumvunjia heshima marehemu.
Mitandaoni, maoni yamegawanyika. Wapo waliomtaka Diana kuacha kutumia urithi wa wasanii wakubwa kama njia ya kujipatia umaarufu, huku wengine wakimtetea wakidai kila msanii ana uhuru wa kuonyesha ubunifu wake kwa namna tofauti.
Hata hivyo, mjadala huu umeonyesha wazi kuwa jina na kazi za E-Sir bado zina nguvu kubwa katika tasnia ya muziki wa Kenya, na zinabaki kuwa urithi unaohitaji kulindwa kwa heshima ya juu