Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

Trevor Amkingia Kifua Diana B Baada ya Ukosoaji wa “Bibi Ya Tajiri”

CEO wa Chama cha Content Creators nchini Kenya, Director Trevor amejitokeza na kumkingia kifua Diana B baada ya kupata ukosoaji mkali kutokana na wimbo wake mpya Bibi ya Tajiri ambao una zaidi ya views laki tano youtube ndani ya siku tatu. Hii ni baada ya baadhi ya mashabiki na wakosoaji wa muziki kudai kuwa Diana hana kipaji cha uimbaji na uandishi wa muziki. Akizungumza, Trevor amewataka Wakenya kumuunga mkono Diana badala ya kumbeza, akisisitiza kuwa kila msanii anastahili nafasi ya kujaribu na kukuza sanaa yake. Aidha, amewataka wasanii wa Kenya kushirikiana naye ili kuendeleza muziki wa ndani badala ya kumpuuza. Trevor, hata hivyo, amesisitiza kuwa huu ni mwanzo wa safari ya Diana katika muziki na kwamba anastahili nafasi ya kuthibitisha kipaji chake. Ukosoaji huo ulianza baada ya mashabiki kudai kuwa Bibi ya Tajiri ilikuwa sampled kutoka wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, Sare Sare. Haikuishia hapo, baadhi walimlaumu Diana kwa kuchana picha za marapa wakubwa nchini kama Khaligraph Jones na Nyashinski kwenye video yake, wakisema kitendo hicho ni kukosea heshima muziki wa hip hop.

Read More
 Mashabiki Wakosoa Diana B kwa Kusample Wimbo wa E-Sir “Saree”

Mashabiki Wakosoa Diana B kwa Kusample Wimbo wa E-Sir “Saree”

Ngoma mpya ya Diana Marua “Bibi Ya Tajiri” imezua mjadala mkubwa baada ya msanii huyo kutumia sample ya wimbo maarufu wa marehemu E-Sir, “Saree”. Ingawa baadhi ya mashabiki waliona hatua hiyo kama heshima kwa nguli huyo wa rap aliyefariki zaidi ya miaka 20 iliyopita, wengi wameibuka na ukosoaji mkali. Wanasema Diana hana uwezo wa kuchana kama E-Sir na kwamba kutumia ngoma hiyo ni sawa na kumvunjia heshima marehemu. Mitandaoni, maoni yamegawanyika. Wapo waliomtaka Diana kuacha kutumia urithi wa wasanii wakubwa kama njia ya kujipatia umaarufu, huku wengine wakimtetea wakidai kila msanii ana uhuru wa kuonyesha ubunifu wake kwa namna tofauti. Hata hivyo, mjadala huu umeonyesha wazi kuwa jina na kazi za E-Sir bado zina nguvu kubwa katika tasnia ya muziki wa Kenya, na zinabaki kuwa urithi unaohitaji kulindwa kwa heshima ya juu

Read More
 VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

VJ Patello Amchana Diana B Baada ya Madai ya Chain Feki

Mzozo kati ya VJ Patello na Influencer aligeukia muziki Diana B umeendelea kuchukua sura mpya baada ya Patello kujibu vikali madai ya kwamba mikufu yake ya dhahabu ni bandia. Kupitia Instagram, Patello alimshutumu Diana na mumewe Bahati kwa kushindwa kulipa shilingi milioni moja kwa Harambee Stars, akiongeza kuwa wawili hao hawana uhalali wa kuzungumzia vitu vya thamani. Ugomvi huo ulianza baada ya Patello kukosoa wimbo mpya wa Diana B uitwao Bibi ya Tajiri, ambapo Diana alisikika akijinadi kuwa ndiye rapa bora nchini Kenya huku akionekana kwenye video akirarua picha za marapa maarufu kama Khaligraph Jones na Nyashinski. Kitendo hicho kilimkera Patello ambaye alimtolea uvivu kwa kudai kuwa hana heshima kwa wasanii halisi wa hiphop, akamtaka aendelee na masuala ya content creation kwa sababu hajui kurap. Diana B hakusita kujibu mashambulizi hayo kwa kumdharau Patello, akisema kwa kejeli kwamba ni ajabu mtu mwenye mikufu bandia anathubutu kukosoa kazi ya “Bibi ya Tajiri”

Read More
 Diana B ashindwa kuficha hisia zake kwa mume wake Bahati

Diana B ashindwa kuficha hisia zake kwa mume wake Bahati

Mwanamitandao aliyegeukia muziki nchini Diana B ameamua kuwapa somo wanawake wa Kenya jinsi ya kuwaonyesha upendo wapenzi zao. Mama huyo wa watoto watatu ameshea video hii kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anamlisha mume wake Bahati ambaye kwa sasa anaumwa. Kwenye posti yake hiyo ameandika ujumbe mzito wa mahaba kwenda kwa mume wake huyo ambaye alionekana kudeka na kitendo hicho huku akimhakikishia kumpenda kwa shida na raha. “In Sickness and in Good Health, Mapenzi Tight kama kifuniko ya gas “, Aliandika. Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kukoshwa na upendo wa wawili hao huku wengi wakiahapa kufuta nyayo zao kwa ajili ya kuboresha mahusiano yao. “Mapenzi wewe any time I pass through dee and bahaa…. I feel I need a man in my life… 2023 wewe lazima mr right akuwe nimechokaa kuangalia ya wenyewe,” Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii aliandika.

Read More
 Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Jalang’o akanusha kutoka kimapenzi na Diana B

Mchekeshaji aliyegeùkia siasa Jalang’o amepuzilia mbali uvumi wa muda mrefu kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mke wa Bahati, Diana B. Kwenye mahojiano na Mungai Eve, Jalango ambaye ni mbunge wa Lang’ata amekanusha madai hayo kwa kusema kwamba uhusiano wake na Diana ulikuwa ni wa kirafiki tu. Aidha amenyosha maelezo kuhusu picha inayosambaa mtandaoni akiwa na Diana kwa kusema kuwa alipiga picha hiyo na mama huyo wa watoto watatu takriban miaka 15 iliyopita alipokutana naye kwenye duka moja la jumla jijini Nairobi. “I remember that photo must have been taken in 10-15 years old at Jamia mall. She requested for a photo and I took a photo with her. I have never dated Diana. Diana has been my friend for the longest time and even when we took that photo it was just a good photo.”, Alisema. Kauli yake imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa wawili hao walikuwa wapenzi kipindi cha nyuma kutokana na hatua ya Diana B kukiri hadharani kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume matajiri kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.

Read More
 Diana B azua gumzo mtandaoni baada ya video yake akikiri kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kusambaa

Diana B azua gumzo mtandaoni baada ya video yake akikiri kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kusambaa

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wametoa maoni mbali kuhusu video ya Diana Marua akiri hadharani kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya pesa. Diana alichapisha video hiyo mwaka 2020 mtandaoni ambapo alidai kwamba kabla ya kukutana na mume wake Bahati alikuwa anachepuka na wanaume wengi kwa lengo la kukidhi mahitaji yake ya msingi. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kipindi ana umri wa miaka 20 pesa haikuwa shida kwake kwani kila mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano naye alikuwa anamhudumia ipasavyo ikiwemo kumlipia kodi sambamba na kumnunulia chakula na mavazi. “I dated guys for money I had people who used to give me 10k, kuna mtu anakupatia 30k, anakupea 20k, nilikuwa na mtu wa kunifanyai shopping ya nyumba , nilikuwa na mtu wa kuni buyia manguo , unajua All I wanted was to live well..”, Alisema Video hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii imeibua hisia mseto miongoni mwa wakenya ambapo wengi wamehoji kuwa Diana B bado ana tamaa ya pesa na huenda akamkimbia bahati ikitokea amefilisika kiuchumi. Hata hivyo wengine wamesema kuwa watu waache kumhukumu mwanamama huyo wa watoto watatu kwa kuwa amebadili mienendo yake ya zamani ikizingatiwa kuwa ametulia na analea familia ya mwimbaji huyo.

Read More
 Diana Bahati aongoza kwa idadi ya subscribers Youtube upande wa wasanii wa kike nchini

Diana Bahati aongoza kwa idadi ya subscribers Youtube upande wa wasanii wa kike nchini

Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana Bahati ametokea kwenye orodha ya wasanii wa kike walio na subscribers wengi barani Afrika. Kwa mujibu wa The Top Chart, Diana B anashikilia nafasi ya 8 akiwa na jumla ya subscribers elfu 783 nyuma ya Zuchu, Yemi Alade, Sinach, Tiwa Savage, Simi na Nandy ambao wanaongoza kwa idadi ya subscribers kwa wasanii wa kike barani Afrika. Kwa matokeo hayo Diana B ndiye msanii anayeongoza nchini kwa idadi ya subscribers kwenye mtandao wa Youtube kwa upande wasanii wa wakike. Diana B ambaye alijiunga na mtandao wa youtube Agosti 19 mwaka 2019, mpaka sasa ana jumla ya watazamaji millioni 119, 452, 136 kupitia kazi zake ambazo anazipakia kwenye mtandao huo.

Read More
 Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Diana B na Bahati watangaza jinsia ya mtoto wao

Couple pendwa nchini inayoundwa na wasanii Diana B pamoja na Bahati imetangaza jinsia ya mtoto wao wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni. Katika hafla ya kutambulisha jinsia ya mtoto huyo wawili hao wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kiumemuda wowote kuanzia sasa Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni mkaribisha mtoto wao wa watatu. Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni kwamba huenda Diana B amejifungua kwa siri kutokana na jumbe zenye ukakasi alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.

Read More
 BAHATI NA DIANA B MBIONI KUPATA MTOTO WATATU

BAHATI NA DIANA B MBIONI KUPATA MTOTO WATATU

Wanandoa mashuhuri nchini Diana Marua na Bahati wamefichua kuwa wanatarajia kupata mtoto wa tatu hivi karibuni. Wakitoa taarifa hiyo njema kwenye chaneli yao ya You Tube, wanandoa hao wamesema kwamba tayari ‘wanampenda’ mtoto wao huyo ambaye hajazaliwa. “kila siku nakutafutia , kwa vile nakulombotov … nakutamkia baraka, nakutakia fanaka, kutoa sadaka nyota yako itawaka, tamka isiyokua na mipaka … malaika wakulinde … na si twakusiburi kama mwisho …” wamesikika wakiimba kwenye video waliyoichapisha chaneli zao za Youtube. Wawili hao wana watoto wawili pamoja, Heaven na Majesty na mashabiki wamewapongeza kwa mafanikio hayo huku wakiwatakia heri wakati huu wanatarajia kumpata mtoto wao wa tatu.

Read More
 DIANA B AMKINGIA KIFUA BAHATI KUFUKUZWA EMBAKASI MASHARIKI

DIANA B AMKINGIA KIFUA BAHATI KUFUKUZWA EMBAKASI MASHARIKI

Mwanamitandao aliyegeukia muziki Diana B amevunja kimya chake mara baada ya mume wake ambaye ni mgombea wa kiti cha ubunge Mathare Kevin Bahati kufukuzwa kwenye mkutano wa kisiasa wa Azimio la umoja huko Embakasi Mashariki, jijini Nairobi. Kupitia Instagram yake Diana B amempa moyo mume wake kwa kusema kwamba aendelee kuipigania ndoto yake kuwa mbunge kwa kuwa wapinzani wameanza kuingiwa na uoga kiasi cha kuanza kumpiga vita kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa mathare baada ya uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu. “You are a force that cannot be ignored!!! The way to the top can never be reached without opposition. keep pushing… God got you, Mathare people already know who is best for them,” Amesema Diana B Kwa upande wake Bahati ameeleza kuwa wapinzani wake waliumizwa na uwepo wake kwenye mkutano huo wa Kisiasa ndiposa wakaamua kufukuza. Hitmaker huyo wa  ngoma ya Adhiambo amedai kuwa waliokuwa wanasimamia mkutano huo walilazimika kusitisha mkutano ghafla licha ya watu kumtaka awahutubie. Hata hivyo katibu wa ODM Edwin Sifuna amesisitiza kuwa mgombea wao wa kiti cha ubunge mathare kupitia azimio la umoja ni Anthony Oluoch, hivyo  bahati aache kutumia  jina lake kutafuta kiki kwani akuhusika kivyovyote kumshurutisha ajiondoe kwenye kinyanganyiro cha ubunge Mathare.

Read More
 DIANA B AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WA MUME WAKE BAHATI

DIANA B AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WA MUME WAKE BAHATI

Mwanamuziki na mtayarishaji wa maudhui nchini Diana Bahati, amemkingia kifua mumewe Kevin Bahati, kwa madai ya kutotumia akaunti yake ya Instagram kwa muda mrefu. Akimjibu shabiki yake aliyetaka kufahamu kiini cha ukimya wa hitmaker huyo wa ngoma Adhiambo diana b kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ukimya wa bahati umetokana na msanii huyo kujikita zaidi kwenye masuala ya kifamilia kwani anatumia muda wake mwingi na watoto wake. Hapo awali, Bahati, alikuwa akiwafahamisha mashabiki wake kuhusu matukio yanayotokea kwenye maisha yake, huku akichapisha maudhui mengi kwenye ukurasa wake ndani ya siku moja. Kwa sasa, ukurasa wa Bahati hauna maudhui mapya tangu alipolia hadharani wiki mbili zilizopita kuhusu masaibu yake ya kisiasa, mara baada ya chama cha jubilee kumpokonya tiketiya kuwania ubunge wa mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu. Tangu wakati huo, mwanamuziki huyo hajachapishaa kitu chochote kipya kwenye mitandao yake ya kijamii akiwaacha mashabiki zake njia panda.

Read More
 DIANA B AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA MKE WA MR. SEED

DIANA B AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA MKE WA MR. SEED

Mwana mitandao aliyegeukia muziki Diana B amekanusha kuwa kwenye bifu na mke wa msanii mwenzake mr. Seed. Akizungumza kwenye ambayo alipewa ubalozi ya hospitali moja jijini Naoirobi, Diana b amekiri kutokuwa na maelewano mazuri na nimo kipindi cha nyuma kwa kusema kwamba hakuwa amekomaa kiakili kushughulikia ugomvi wao kiustaarabu. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mubaba” ameongeza kuwa yeye na Nimo walikuwa hawajakutana kwa muda mrefu lakini kwa sasa wana maelewano mazuri baada ya kuweka kando tofauti zao “Tofauti zilikuwepo lakini unajua watu hufanya makosa katika miaka yao nyuma na wakati mwingine unagundua labda haujakomaa kiaki kushughulikia maswala fulani kwa njia bora lakini maisha hutufundisha somo,” alisema. Diana na Nimo waliingia kwenye ugomvi mwaka wa 2018 wakati wa sherehe za Mwaka Mpya ambapo Diana alidaiwa kumdhulumu Nimo vibaya licha ya kuwa mjamzito kipindi hicho.

Read More