
Dansa maarufu nchini Tanzania Angel Nyigu amefunguka kwa hisia kali baada ya msanii wa Bongo Fleva, Zuchu, kudai kuwa Ashurey ndiye dansa namba moja Afrika Mashariki. Kauli hiyo imeonekana kumkera Nyigu, ambaye amesema Ashurey bado ni mtoto mdogo na hajafikia viwango vya kupewa heshima hiyo kubwa katika tasnia ya densi.
Angel Nyigu aliongeza kuwa umaarufu wa Ashurey unatokana zaidi na brand ya Zuchu inayombeba, na si kwa uwezo wake binafsi wa kucheza densi. Ameeleza pia kuwa yeye ndiye aliyemtambulisha Ashurey kwa Zuchu, lakini tangu wakati huo uhusiano wao haujawahi kuwa mzuri baada ya Ashurey kumblock bila sababu za msingi.
Kauli hizi zimezua gumzo mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wamejitokeza kumtetea Angel Nyigu kwa kudai ana uzoefu mkubwa na mchango wake hauwezi kupuuzwa, huku wengine wakisema Ashurey amejitengenezea jina kutokana na jitihada zake na ushirikiano wake wa karibu na Zuchu