
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, ameibua mjadala baada ya takwimu kuonyesha kuwa muziki wake unasikilizwa zaidi nchini Kenya kuliko nyumbani kwao Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za YouTube, nyimbo za Mbosso zimeangaliwa zaidi ya mara milioni 102 kutoka Kenya, ikilinganishwa na mara milioni 47 kutoka Tanzania. Hii inamaanisha kwamba takribani asilimia 68.5 ya watazamaji wake kutoka Kenya na Tanzania wanatoka Kenya pekee.
Ufanisi huu unaonyesha namna Mbosso alivyojijengea mashabiki wakubwa nchini Kenya, huku muziki wake ukiendelea kushika nafasi kwenye redio, majukwaa ya kidijitali na mitoko ya burudani.
Wachambuzi wa muziki wanasema hali hii inathibitisha nguvu ya soko la Kenya kwa wasanii wa Afrika Mashariki, na kwa Mbosso, inaweza kufungua milango ya ushirikiano zaidi na wasanii wa Kenya pamoja na kuongeza idadi ya shoo katika nchi hiyo.