Gossip

Kauli ya Vera Sidika Yazima Uvumi wa Kurudiana na Brown Mauzo

Kauli ya Vera Sidika Yazima Uvumi wa Kurudiana na Brown Mauzo

Socialite maarufu wa Kenya, Vera Sidika, amezima madai yanayoenezwa mitandaoni kuwa anapanga kurudiana na mzazi mwenzake, mwanamuziki Brown Mauzo licha ya kuendelea kushirikiana naye katika malezi ya watoto wao.

Kupitia ujumbe aliouweka kwenye Instagram, Vera amekanusha vikali uvumi huo na kueleza kuwa maamuzi yake yamelenga tu kuhakikisha watoto wao wanapata malezi bora. Amesisitiza kwamba hatua ya kuruhusu Brown kuwa karibu na watoto wao haimaanishi kuwa anataka kurejesha mahusiano, bali ni kutambua wajibu wake kama baba.

Mwanamama huyo pia amewakumbusha mashabiki wake kuwa alishawahi kuandaa “divorce party” kama alama ya kufunga ukurasa wa ndoa yake na Mauzo, jambo analosema linatosha kuonyesha kuwa hawezi kurudiana naye.

Hii inakuja baada ya mijadala kuzuka mitandaoni, mashabiki wakidai kitendo chake cha kumruhusu Brown Mauzo kuja nyumbani kwake na kukaa na watoto wao ni ishara ya wawili hao kutaka kufufua uhusiano wao wa kimapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *