Entertainment

Kauli ya Kiroho ya Mavokali Yaacha Mashabiki na Maswali

Kauli ya Kiroho ya Mavokali Yaacha Mashabiki na Maswali

Msanii wa Bongofleva, Mavokali, ameacha mashabiki wake wakijiuliza maswali baada ya kutoa ujumbe mzito wenye maudhui ya kiroho, uliojaa sala na toba kwa Mungu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mavokali ameonekana kujiweka kwa unyenyekevu mbele za Mungu, akisema kwamba hana nguvu ya kutimiza maagizo yote ya kiimani, ila anaomba rehema na msamaha kwa dhambi anazozifanya kwa siri.

Katika kauli yake, Mavokali amesema kwamba siku atakapoitwa mbele za haki, anamuomba Mungu ampoke pamoja na madhaifu yake, amstiri kwa rehema na kumpunguzia maumivu ya umauti. Hitmaker huyo wa Komando, ameongeza kuwa anahisi aibu kufika mbele za Muumba akiwa na rundo la dhambi, lakini anaamini rehema za Mungu ndizo zitakazombeba.

Maneno hayo yamewagusa mashabiki wake wengi, huku baadhi wakiyatafsiri kama sala binafsi ya msanii huyo, na wengine wakiamini huenda ni sehemu ya lyrics za wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *