Socialite anayesuasua nchini Kenya, Pritty Vishy, ameanikwa mtandaoni na rafiki yake wa karibu kuwa alifanya upasuaji wa kuongeza makalio (BBL) kwa siri licha ya kukana mara kwa mara.
Kwa mujibu wa rafiki yake Becky Akinyi, Pritty alifanyiwa upasuaji wa BBL na kwamba alihusika kumsaidia na kumhudumia wakati alipokuwa kwenye mchakato wa kupona baada ya upasuaji huo.
Akinyi amemtaka Pritty Vishy kuacha kuwadanganya wakenya kuhusu mabadiliko ya mwonekano wake ilhali alifanya upasuaji wa kuboresha mwili wake.
Kauli ya Becky imewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa hapo awali Pritty Vishy alikuwa akikanusha mara kwa mara madai ya kufanyiwa upasuaji wa urembo, akisisitiza kuwa mabadiliko ya mwili wake yalitokana na mazoezi na mtindo wa maisha.