
Mwanamuziki Bien, kutoka kundi la Sauti Sol, ameweka wazi mtazamo wake kuhusu ndoa akisema kwamba ni jambo zuri na lenye manufaa kwa mtu binafsi na hata kwa jamii.
Akipiga stori na SPM Buzz, Bien amesema kuwa licha ya kuwepo kwa mitazamo tofauti kutoka kwa watu wengine, yeye anaamini ndoa inaleta ukuaji wa kweli katika maisha ya mtu. Ameeleza kuwa watu wanaoona ndoa kama mzigo au kizuizi wanakosea, kwani yeye mwenyewe ni mfano hai wa mafanikio na mabadiliko chanya yanayotokana na ndoa yake.
Kwa mujibu wa msanii huyo, ndoa siyo kikwazo cha maendeleo kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu, bali ni chanzo cha baraka na chachu ya ukuaji wa mtu binafsi na kifamilia.
Kauli ya Bien imekuja baada ya socialite wa Kenya, aitwaye Chebet Rono, kuzua mjadala mitandaoni akidai kuwa ndoa hubamba mafala. Kauli ambayo iliibua hisia mseto, huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakijadiliana kwa mapana kuhusu mustakabali na maana ya ndoa kwa vijana wa kizazi cha sasa.