LifeStyle

Presenter Ali Afunguka Kuhusu Uvumi wa Kutengana na Medina

Presenter Ali Afunguka Kuhusu Uvumi wa Kutengana na Medina

Content creator kutoka Kenya, Presenter Ali, ameweka wazi msimamo wake kufuatia uvumi ulioenea mitandaoni kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mkewe, Medina.

Akipiga stori na Oga Obinna, Ali amesema kuwa hali ya ndoa yao haipaswi kuwa mjadala wa umma. Amefafanua kuwa si kweli kwamba wameachana, na pia si sahihi kudhani bado wako pamoja kwa misingi ya kile mashabiki wanaona mitandaoni.

Amesisitiza kuwa maisha yake ya kifamilia ni jambo binafsi, na kwamba watu hawapaswi kulazimisha majibu kwa masuala ambayo hayawahusu.

Uvumi wa kutengana kwa wawili hao ulianza baada ya mashabiki kugundua kuwa Ali na Medina wameacha kufuatana kwenye mitandao ya kijamii.

Sanjari na hilo, Ali hakuchapisha ujumbe wa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mkewe, jambo ambalo alikuwa akifanya kila mwaka, hali iliyozidisha minong’ono kuwa huenda ndoa yao imeingia na ukungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *