
Mwanamuziki Bien, ambaye zamani alikuwa mwanachama wa kundi la Sauti Sol, ameibuka kinara katika orodha ya wasanii wa Kenya wanaotazamwa zaidi kwenye YouTube kwa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa YouTube Charts Kenya, Bien amefikisha jumla ya watazamaji milioni 78.7, akithibitisha nafasi yake kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya.
Akimfuata kwa karibu ni msanii wa ohangla Prince Indah aliyepata watazamaji milioni 64.7, huku Willy Paul akishika nafasi ya tatu kwa jumla ya watazamaji milioni 61.9. Otile Brown naye aliorodheshwa katika nafasi ya nne baada ya kupata watazamaji milioni 55.3, akionyesha kuwa bado ni miongoni mwa wanamuziki maarufu zaidi nchini humo.
Wachambuzi wa burudani wanasema ukuaji wa takwimu hizi unaonyesha jinsi mashabiki wa muziki nchini Kenya wanavyotumia YouTube kama jukwaa kuu la kusikiliza na kutazama kazi za wasanii wao wa nyumbani, jambo linaloongeza ushindani na kuimarisha tasnia ya muziki wa Kenya.