Entertainment

Daddy Owen Afunguka Kuhusu Tukio Lililomvunja Moyo Akiwa Kwenye Kilele cha Umaarufu

Daddy Owen Afunguka Kuhusu Tukio Lililomvunja Moyo Akiwa Kwenye Kilele cha Umaarufu

Msanii wa nyimbo za injili nchini Kenya, Daddy Owen, amesimulia kisa cha kusikitisha alichowahi kupitia akiwa kwenye kilele cha umaarufu kisanaa.

Akiwa kwenye mahojiano hivi karibuni, Owen ameeleza jinsi alivyokuwa amialikwa kutumbuiza katika shule moja ya wasichana, lakini aliposhika jukwaa, wanafunzi wote walitoka ukumbini na kumwacha peke yake. Tukio hilo lilisababishwa na tetesi zilizokuwa zikienea wakati huo zikimhusisha na ibada za kishetani.

Daddy Owen amesema kitendo hicho kilimuumiza, lakini kilimjenga na kumpa moyo wa kuendelea na huduma yake ya injili kupitia muziki. Ameongeza kuwa changamoto kama hizo ni sehemu ya safari ya imani na sanaa, akisisitiza umuhimu wa kusimama imara licha ya madai ya uongo.

Kisa hicho kilitokea wakati msanii huyo alikuwa kwenye kilele cha muziki wake, ambapo vibao vyake maarufu kama System ya Kapungala na Tobina vilikuwa vikivuma sana na kumpa umaarufu mkubwa nchini. Licha ya changamoto hizo, Daddy Owen ameendelea kung’ara kama mmoja wa wanamuziki wa injili wenye ushawishi mkubwa nchini, akiwa na nyimbo nyingi zenye ujumbe wa matumaini na uvumilivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *