Entertainment

Joel Lwaga Asaini Mkataba na Empire Africa

Joel Lwaga Asaini Mkataba na Empire Africa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania, Joel Lwaga, ametangaza rasmi kusaini mkataba wa usambazaji wa muziki na kampuni kubwa ya kimataifa, Empire Africa. Hatua hii imeonekana kama mwanzo mpya wa ushirikiano wa kibiashara ambao unatarajiwa kupeleka muziki wake katika viwango vya juu zaidi na kumfikisha kwa mashabiki wengi duniani.

Kama ishara ya mwanzo wa safari hii mpya, Lwaga ameachia wimbo wake mpya unaoitwa “Saa Hii”, ambao tayari upo kwenye majukwaa yote ya kidigitali duniani. Wimbo huo unakuja na ujumbe wa imani na matumaini, ambao ni utambulisho wa kipekee wa muziki wa Joel Lwaga.

Mashabiki wake wamepokea kwa furaha tangazo hilo, wakieleza matumaini makubwa kwamba ushirikiano huu na Empire Africa utaleta mafanikio makubwa zaidi kwa msanii huyo anayejulikana kwa sauti yake yenye kugusa mioyo na nyimbo zenye ujumbe wa kiroho.

Kwa kusaini mkataba huu, Joel Lwaga anaungana na orodha ya wasanii kutoka barani Afrika wanaofanya kazi na Empire Africa, kampuni ambayo inajulikana kwa kufanikisha kazi za wasanii katika soko la kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *