Entertainment

Dayoo Aachwa na Meneja Wake Baada ya Kuuza Haki za Muziki Wake

Dayoo Aachwa na Meneja Wake Baada ya Kuuza Haki za Muziki Wake

Meneja wa muziki kutoka Tanzania, Mnene, ameweka wazi sababu kuu iliyomfanya kusitisha kazi yake ya usimamizi wa msanii Dayoo.

Akipiga stori na Rick Media, Mnene amesema moja ya mambo yaliyomvunja moyo ni hatua ya Dayoo kuuza umiliki wa kazi zake za muziki (catalogue) bila kushirikisha timu yake ya usimamizi.

Kwa mujibu wa meneja huyo, uamuzi wa Dayoo kuachia haki za umiliki wa nyimbo zake ulikuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa kazi zao za pamoja, jambo lililosababisha migongano ya kimaslahi.

Hata hivyo, Mnene amesisitiza kuwa anaendelea kumtakia Dayoo mafanikio katika safari yake ya muziki, licha ya kutengana kikazi. Kwa sasa, Meneja Mnene amesema ataendelea na mipango yake ya kusimamia vipaji vingine huku akisisitiza kuwa anaamini katika uwekezaji wa muda mrefu kwenye kazi za muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *