
Mchekeshaji wa Kenya, Terence Creative, ameweka wazi safari yake ya kupambana na uraibu wa vileo, akifichua jinsi alivyoingia katika wakati mgumu maishani mwake kabla ya kurejea katika mstari sahihi.
Akiangazia kipindi hicho kigumu, Terence amesema changamoto za uraibu wa pombe na uvutaji sigara zilimpelekea kupoteza mwelekeo na matumaini, lakini hakubaki peke yake. Amemshukuru mkewe Milly Chebi ambaye kwa wakati huo alikuwa mpenzi wake kwa kusimama naye na kumsaidia kuvuka kipindi cha giza katika maisha yake.
Terence ameeleza kuwa upendo na uvumilivu wa mkewe ndiyo uliokuwa nguzo muhimu ya safari yake ya kupona na kupata nafasi mpya ya kuanza upya. Aidha, ametumia hadithi yake kuhamasisha wengine wanaokabiliwa na changamoto za uraibu kutafuta msaada na kutokata tamaa.
Hata hivyo ametoa ushauri kwa vijana, akiwahimiza kufanya maamuzi sahihi wanapochagua wapenzi. Amesisitiza kuwa si kila mtu anaweza kusimama na mpenzi wake katika nyakati ngumu, hivyo vijana wanapaswa kuchukua tahadhari na kuchagua wenza watakaowaunga mkono kwa dhati.