Entertainment

Victoria Kimani Asema Ukimya wa Mashabiki Unakatisha Tamaa

Victoria Kimani Asema Ukimya wa Mashabiki Unakatisha Tamaa

Mwanamuziki wa Kenya, Victoria Kimani, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kulalamikia zaidi ya watazamaji 25,000 wa Insta Story zake wanaoangalia maudhui yake bila kuonyesha ushirikiano wowote.

Kupitia Instastory yake Instagram, Kimani amesema hali hiyo inamfanya ajihisi kupuuzwa licha ya watu wengi kutazama maudhui yake. Ameongeza kuwa hali ya kuwa na watazamaji wengi kimya inamfanya aone kama juhudi zake hazithaminiwi ipasavyo.

Kupitia ujumbe wake, ametoa pia wito kwa mashabiki wake kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi kwa kuonyesha mapenzi yao kupitia likes, maoni na ku-share au kushiriki maudhui yake.

Mrembo huyo amesisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu kwa wasanii kwa sababu huwapa motisha ya kuendelea kutoa kazi bora na kuendeleza uhusiano wa karibu na wafuasi wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *