Victoria Kimani Adai Kutojua Lugha Hiyo ni Baraka Kutoka kwa Mungu
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Victoria Kimani, amezua sintofahamu mtandaoni baada ya kutoa kauli inayotafsiriwa na wengi kama dharau dhidi ya lugha ya Kiswahili. Kupitia Instastory, msanii huyo amedai kuwa kutokujua Kiswahili kumemsaidia kulinda afya yake ya akili. Victoria Kimani, ambaye amekuwa akikosolewa kwa miaka mingi kwa kutumia lugha ya Kiingereza katika kazi zake, ameeleza kuwa kutokuimudu lugha ya Kiswahili ni baraka kutoka kwa Mungu. Kwa mujibu wa msanii huyo, hali hiyo imekuwa kinga tosha dhidi ya mashambulizi ya maneno na dhoruba za matusi ambazo mara nyingi huelekezwa kwa wasanii kupitia lugha hiyo. Kauli yake imekuja kama majibu ya shinikizo la muda mrefu kutoka kwa mashabiki wake, ambao wamekuwa wakimhimiza kuimba kwa Kiswahili ili kuimarisha utambulisho wake kama msanii wa Kiafrika. Mashabiki wengi wanahisi kuwa kutumia lugha ya kigeni pekee kunamfanya aonekane kama msanii wa Kimarekani zaidi kuliko Mkenya.
Read More