Entertainment

Msanii Chipukizi Pipi Jojo Kutambulisha EP Mpya Oktoba 9

Msanii Chipukizi Pipi Jojo Kutambulisha EP Mpya Oktoba 9

Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi, Pipi Jojo, ametangaza kuwa ataachia rasmi EP yake mpya Oktoba 9 kwenye majukwaa yote ya kidigitali.

Kupitia ujumbe wake, Pipi Jojo ameeleza kuwa alipata nafasi ya kukutana na Chief Godlove Billionaire kwa ajili ya kumsikilizisha kazi zake, ambapo kwa bahati nzuri alikutana pia na gwiji wa muziki wa HipHop nchini Tanzania, Chid Benz.

Amesema kuwa kukutana na Chid Benz kumekuwa ni heshima kubwa kwake, kwani mbali na kupata ushauri wa kitaalamu, hakutarajia kuwa msanii mkongwe wa hadhi hiyo angekubali na kubariki kazi zake.

Kwa mujibu wa Pipi Jojo, wawili hao walimsikiliza kwa makini na kumpa baraka ya kuachia rasmi kazi zake, jambo ambalo amelitaja kuwa ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki.

Ameomba mashabiki, vyombo vya habari na wadau mbalimbali wa muziki kumpa sapoti ili EP yake ipokelewe vyema sokoni na kumsaidia kusonga mbele katika ndoto yake ya kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *