
Msanii wa Singeli, Dulla Makabila, ametoa ushauri mzito kwa vijana wenzake ambao bado hawajafanikwa kimaisha lakini wako kwenye mahusiano.
Kupitia ujumbe wake Instagram, Dulla Makabila amesema kuwa iwapo kijana hana fedha kwa sasa na mwanamke wake anaonyesha uvumilivu na kuendelea kusimama naye, basi asiruhusu kumpoteza mwanamke huyo kwa sababu ya mapungufu madogo aliyo nayo.
Msanii huyo, amefafanua kuwa katika safari ya maisha, ni vigumu sana kwa mtu aliyefanikiwa kifedha kugundua mwanamke anayempenda kwa dhati na yupi anayempenda kwa ajili ya pesa zake.
Kwa mtazamo wa msanii huyo, mwanamke anayechagua kubaki na mwanaume katika kipindi kigumu cha maisha ni wa thamani kubwa, kwani anathibitisha mapenzi ya kweli na sio ya kimaslahi.