Sports news

Timu ya Vijana Ya Baseball5 Ya Kenya Yazidi Kushangaza Dunia

Timu ya Vijana Ya Baseball5 Ya Kenya Yazidi Kushangaza Dunia

Timu ya taifa ya vijana ya mpira wa Baseball5 ilipokelewa kwa shangwe katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ilipowasili nyumbani baada ya kuandikisha historia kwa kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya dunia ya vijana ya WBSC Baseball5 mjini Nayarit, Mexico.

Kenya ilianza kampeni hiyo kwa changamoto baada ya kufungwa na mabingwa wapya wa dunia, Cuba, lakini walirejea kwa nguvu mpya waliposhinda mechi dhidi ya Korea na Tunisia kwa seti 2-0 kila mmoja. Baadaye, walitoka na ushindi wa seti 2-1 dhidi ya Uhispania na kufuzu robo fainali, ambapo walikubali kufungwa na wenyeji Mexico.

Kwa mara ya kwanza kushiriki mashindano hayo ya dunia, Kenya ilitawazwa timu bora barani Afrika, jambo lililoipa heshima kubwa na kuwahamasisha vijana wengi nchini kujiunga na mpira wa Baseball5. Mafanikio haya ni ushahidi wa ukuaji wa mchezo huo unaochipuka katika nchi yetu.

Mashabiki na wadau wa mchezo wa Baseball5 wanatarajia timu ya Young Falcons kuendelea kuonyesha umahiri zaidi katika mashindano yajayo, huku wakiahidi kuendeleza ushindi na kuleta heshima zaidi kwa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *