LifeStyle

Moya David Aanza Safari ya Gym Baada ya Mashabiki Kumshauri Apunguze Kitambi

Moya David Aanza Safari ya Gym Baada ya Mashabiki Kumshauri Apunguze Kitambi

Dansa maarufu mitandaoni kutoka Kenya, Moya David, ameanza rasmi safari yake ya mazoezi ya gym kufuatia shinikizo la mashabiki waliomtaka apunguze uzito.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Moya aliposti picha akiwa gym na kuambatanisha ujumbe akisema ni siku yake ya kwanza kufanya mazoezi.

Amefichua kuwa mashabiki wengi wamekuwa wakimshauri kupunguza kitambi, akisisitiza kuwa ni kazi ngumu, lakini sasa hana kisingizio baada ya shabiki wake wa dhati, Veronicah Wairimu, kumlipia uanachama wa gym kwa gharama ya KSh 31,700.

Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake mitandaoni, wengi wakimtia moyo kwa uamuzi huo na kumpongeza Veronicah kwa ukarimu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *